MILLION DOLLAR HABITS by BRIAN TRACY

By | September 22, 2018

*Introduction*

Hivyo ulivyo ni kutokana na unayoyafanya:
Katika kitabu hiki kwanza mwandishi wa kitabu hiki anasema kwamba watu waliowengi dunia wapo vile ni kutoka na yale wanayoyafanya kila siku,
Mwandishi anaenda kutueleza kuhusu faida za mazoea/tabia mbalimbali jinsi zinavyoweza kuathili maisha ya mtu au maendeleo ya watu.mwandishi anasema hii ndio siri ya mafanikio kuwa na tabia za kimafanikio
Mwandishi anasema yeye miaka mingi iliyopita alijiuliza *”kwa nini baadhi ya watu ni matajiri na wanamafanikio makubwa kuliko wengine!?* ” Hapa ndipo akaanza kufanya utafiti na kusoma vitabu vingi mno ili kupata siri iyopo kwenye hiyo tofauti katika biashara,saikolojia,kidini,kihistoria na kiuchumi baada ya muda akaanza kupata majibu ya utafiti wake na anasema kwamba “**upo hapo ulipo kwa sababu ya wewe mwenyewe ndio umeamua kuwa hapo**
Tupo hivi tulivyo leo au tukavyokuwa huko mbele kwenye maisha yetu yajayo hii ni kutoka na sisi wenyewe.Maisha yetu ya leo ni kutokana na jumla ya matokeo ya uchaguzi,maamuzi na matendo kutoka siku ya leo kurudi nyuma na kipindi kilichopita,
Tunaweza kutengeneza maisha yetu yajayo kwa kubadili tabia zetu,pia tunaweza kuchagua maamuzi ambayo yanaweza kutupeleka pale tunapo pataka kuwepo au tuna maono napo!

*Power of habit* (nguvu ya tabia)
Mwandishi anasema 95% ya mambo unayofikiria,unayojisikia kufanya na yale unayoyapata ni kutokana na tabia zako.
Lakn mwandishi kifupi anasema kwamba watu wenye mafanikio huwa wanatabia za kimafanikio na wale ambao hawana mafanikio pia wanatabia za kutokuleta mafanikio,kwa hiyo wale wenye tabia za mafanikio ndio wanafanikiwa zaidi kulinganisha na kundi hili jingine!
*Nini maana ya mafanikio??* (defn of success)
Mwandishi anasema kwa upande wake maana ya mafanikio *ni ule uwezo wa mtu kuishi maisha anayoyataka,kufanya mambo ambayo anayafurahia,na kuzungukwa na watu ambao wanakukubali na kuheshimiwa.*
Pia mwandishi anasema kwamba neno mafanikio lina tofautiana kwa kila mtu lakini kuna mambo manne ambayo kila mtu lazima huwa anahitaji ili afanikiwe mambo hayo ni
1.Kuwa na afya njema.
Kila mtu anapenda kuishi bila maumivu au kuumwa na magonjwa kwa hiyo kila mtu anahitaji kuwa na afya njema.
2.Mahusiano bora
Kila mtu anahitaji kuwa na mahusiano yaliyo mema,yenye amani katika jamaii inayomuzunguka,marafiki,kila mtu anpendwa kuheshimiwa kupendwa na 85% ya furaha yako huwa inatokana na ubora wa mahusiano kati yako na jamii kiujumla
3.fanya unachokipenda
Mwandishi anasema watu wanaofanya wanachokipenda huwa na furaha na pia anasema kupitia kitabu hiki utajifunza mambo ambayo watu waliofanikiwa wanavyofanya na wewe ufanikiwe.
4.Kujitegemea katika masuala ya fedha/kiuchumi.
Kila mtu anapenda kuwa huru na kuwa na fedha ambayo inaweza kutatua shida zake na hapa mwandishi anasema kwamba mfano mtu akienda mgahawani au hotelini basi anakuwa anaangalia ile menyu upande wa chakula anachohitaji na siyo upande wa kulia ambako ndio kuna gharama za hiko chakula.
Mwandishi anasema kwamba kila tabia ni yakufunzwa kwa hiyo mtu yeyote anaweza kuwa bora na mwenye mafanikio ikiwa atajifunza tabia za kuleta mafanikio. Mwandishi natoa mfano wa millionea wa kwanza *Benjamin Franklin* ambaye alijifunza tabia ya wema kwa sababu alikuwa mkaidi na akaanza kuwa na tabia njema kwa wafanyakazi wenzake.
Mwandishi anasema wewe ndio unayeweza kudhibiti mienendo yako,anasema kuwa na tabia mbaya ni rahisi kuzijenga lakini ni ngumu kuishi na tabia mbaya!,tabia nzuri ni ngumu kuzijenga lakini ni rahisi kuishi na tabia nzuri.

“We first make our habits,and then our habits make us”.(john Dryden)
@Jackson mwanyika
Phone no.0742364499
Email.mwanyikajackson428@gmail.com

Ahsante ,
Usikose kupata sura ya kwanza ya kitabu kesho!
Barikiwa

Leave a Reply