TIMIZA MALENGO YAKO

By | July 14, 2018

Utafiti mmoja uliofanyika kuhusu tabia za watu wanaofanikiwa uligundua kuwa moja ya tabia muhimu sana ni “Uwezo wako wa Kutawala Hisia
Zako”.Katika watu 100 waliofanikiwa ilionekana kuwa 94 kati yao walisema uwezo wako wa kutawala Hisia zako ni nguzo muhimu ya mafanikio.
.
Katika kufukuzia ndoto zako unatakiwa kujua kuwa sio kila wakati unatakiwa kuonyesha hasira/Kuzungumza au kupambana-Huwa inategemea.
.
1)HISIA UNAPOKATALIWA:Watu wengi sana wameshindwa kuendelea hatua za mbele kwa sababu waliwahi kukataliwa wakati fulani
kwenye maisha yao.Unachotakiwa kujua ni kuwa kukataliwa mara moja hakukufanyi kushindwa milele.Jifunze KUSAHAU kukataliwa na
usiruhusu kujiona hauna THAMANI kwa sababu uliwahi kukataliwa.
.
2)HISIA ZA HASIRA:Kuna watu waliwahi kuruhusu Hisia zao ziwatawale na wakasema Kitu ama kufanya kitu kilichowagharimu maisha yao
yote.Kumbuka kuwa kuna wakati utalazimika kujizuia kufanya ama kusema sio kwa sababu HAUNA NGUVU ila ni kwa SABABU SIO KITU
SAHIHI KUFANYA.Usisahau kuwa Kuwa KIMYA NALO NI JIBU.
.
3)HISIA UNAPOSONGIZIWA:Kuna watu wamepitia mateso katika maisha yao kwa kuadhibiwa ama Kutuhumiwa vitu ambavyo
hawajafanya.Wengi hali hii imewafanya waishi kwa UCHUNGU sana kuona kama hawana thamani.Kumbuka Yusufu kwenye biblia alisingiziwa
amebaka na akagundua lakini mwisho wa siku alikuja kuwa waziri mkuu bila kufanya kampeni.Usiruhusu magumu uliyoyapitia kwa
kusingiziwa,YAUE NDOTO YAKO.Amka,songa mbele!
.
Je,Kuna HISIA yoyote kati ya hizi umeshawahi kupitia???

DOWNLOAD HIPA APP KWENYE PLAYSTORE

Leave a Reply