MILLION DOLLAR HABITS by BRIAN TRACY

By | September 22, 2018

SURA YA PILI,
*MPANGO MKUU WA MAFANIKIO*
👉🏻Siri ya mafanikio ni kujua hatima yako na baada ya kujua hatima yako ndipo uanze kufanya mambo kulingana na kujua ile hatima yako.
👉🏻Swali la kujiuliza kuhusu mafanikio ni vipi utangundua unayoyafikiria muda mwingi katika maisha ya yako na pia kwa nini watu wengine wanakuwa na mawazo chanya na yenye kujenga na wanakuwa na mipango ya mafanikio wakati wengine hawako hivyo,
👉🏻Mwandishi anasema watu wengi waliofanikiwa walipo ulizwa swali kwamba *vitu gani wanafikiria muda mwingi katika maisha yao* ? Anasema kifupi ni kwamba majibu yalikuwa wao wanafikiria kuhusu mambo wenye uhitaji nayo na watapataje hayo wanayohitaji katika huo muda mwingi.Lakini watu wasio na mafanikio wao wanafikiria vitu ambavyo hawavipendi muda mwingi na wanachukia matatizo yao na magumu wanayopitia.
👉🏻Kutoka na ile sheria ya uvutano tuliopitia jana kwenye sura ya kwanza sheria hii huwa ipo katika (neutral) kwa hiyo kutokana na kwamba hawa ambao hawana mafanikio kuchukia matatizo basi wanajikuta matatizo yana ongezeka kwao na wale wenye mafanikio basi wnavutia mafanikio kwao.
👉🏻Dhana binafsi au kujiona mwenyewe ulivyo ndani yako, kama utakuwa umeweka dhana chanya katika eneo fulani au kwa kitu fulani unachotaka kufanya badae na ukatumia dhana hiyo ndani yako na ukajiona tayari umeshakuwa ulivyokuwa unatamani kuwa hivyo utaanza kufanya mambo kulingana na mahitaji yako.
Mfano,kuwa na dhana binafsi unamvuto kiasi gani kwa jamii ndivyo utakapo jiweka ili uwe na mvuto na hii itakusaidia wewe kuwa kama unavyohitaji kuwa na mvuto.
👉🏻Kulidhika mapema na mazoea mabaya,siku zote mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa na siyo wakawaida ila mazoea na kulidhika mapema kunaweza fanya mtu kuwa wakawaida kama watu wengine, mtu anayepanga mambo yake kwa ukubwa zaidi atafanyakazi na kutoa muda mwingi kulifanya jambo mpaka ahakikishe analimaliza,ila mtu akipanga jambo dogo na akamaliza mapema hawezi kujishughulisha tena,mfano mtu akipanga kupata milioni 5 kwa mwaka atafanya kazi mpaka afikishe ile fedha na mtu akipanga afikishe milioni 20 kwa mwaka lazima atafikisha na akifikisha basi hawezi kufanya juhudi kuongeza tena zaidi ya hiko kiasi,kwa hiyo sasa mazoea inabakikuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio na kufanya mambo makubwa,ili kutoka kwenye mfumo wa mazoea unatakiwa kubadili dhana binafsi na kubadili tabia kufanya mambo makubwa zaidi.
👉🏻Jitengenezee mwenyewe mipango mikubwa ya mafanikio, kuna usemi usemao kwamba kwenye udaktari *utambuzi mzuri kwa mgonjwa ni nusu ya kumponya mgonjwa*
👉🏻Dhana binafsi imegawanyika katika sehemu tatu na tuone jinsi hizi sehemu zinavyoshirikiana kila moja na zinafanyaje kazi ilikufanya na kukuwezesha unachokitaka.
1.Ubora wako binafsi, hapa ni ile picha ambayo wewe binafsi unajiona,unaweza ukawa unajiona ni mtu mwenye mafanikio makubwa mno hata kama upo katika mazingira magumu kiasi gani,
Ubora wako binafsi mara nyingi unajengwa na ndoto,malengo na nk kuhusu maono yajayo,ikijumuishwa na ubora na mambo mema ambayo wewe unayakubali na kwa watu wanaokuzunguka.Na watu waliofanikiwa huwa wanajua ubora wao wenyewe binafsi.
Pamoja na kwamba utakuwa na picha ya ubora ubinafsi ndani yako unahitaji haya;-
💜unahitaji kuwa na watu kama mwongozo wako ambao wao ni chanya kwako na wakusaidie kukutengeneza vizuri.
💜Unahitaji kutengeneza vizuri utu wako,unatakiwa kujua thamani yako na unatakiwa kuhakikisha unatengeneza utu wako ili ufanikiwe zaidi na zaidi,thamani yako itakuja pale utakapokuwa unafikiria kile unachokihitaji wakati ujao na kwa sababu ya kanuni ya uvutano lazima kile unacho kihitaji kitakuja kwako.
2.Unajionaje wewe binafsi, kuna mwandishi mmoja wa kitabu kinaitwa PSYCHO-CYBERNETICS kimeandikwa na Dr.MAXWELL MALTZ,tunajifunza kwamba mara nyingi mtu alivyo kwa ndani huoneshwa na yale aliyotenda kwa nje!,kama utajiona kwa ndani ni chanya,maarufu na mwenye mafanikio ndani yako, hivyo ndivyo utakavyoweza kufanya mambo kwa nje,( kwenye ulimwengu wa kawaida)
Dhana yako binafsi huwa inatwa *kioo cha ndani yako* na kioo hiki huwa kinaonesha uhalisia wako kabla hujaamua kufanya jambo fulani katika maisha yako,
Mfano ,kama unajiona mwenyewe ni mtu wakujiamini na unamafanikio kabla hujaonana na mtu mpya,kazi mpya au kufanya mkutano fulani basi ndivyo itakavyokuwa kwenye ulimwengu wa kawaida, kwa hiyo mojawapo ya tabia ambazo ni muhimu kuzijenga ni hii yakujiona tayari uko vizuri kabla hujafanya jambo fulani.
3.kujiheshimu binafsi,unapojiheshimu na kujikubali binafsi hii inakupa nguvu kwa utu wako na kuongeza ufanisi wako wakufanya mambo ambayo umeyapanga.Wasaikolojia wamekubaliana na ukweli kwamba kujikubali binafsi ni sehemu kubwa ya utu wa mtu na mara nyinyi unaweza ukagundua na kutumia kujua kwamba utakuwa na mafanikio au kushindwa kuwa na mafanikio.
👉🏻Ukweli kwamba ni kwamba unapojikubali mwenyewe binafsi ni muhimu zaidi kwa sababu inasaidia kupanga maisha yako kwa ufanisi
👉🏻Kuna kanuni moja inaitwa KILA KITU KINAHESABIKA ni kwamba kila kitu kinachokutokea na kila kitu kinacho kuzunguka kina athari katika kujikubali kwako kwa namna fulani.kwa hiyo kila kitu kinachotokea kwako huwa kinaweza kushusha au kuongeza kujikubali kwako.
👉🏻Linganisha tabia yako na ubora wako,mojawapo ya mambo muhimu ni kwamba umbali kati ya picha yako binafsi, vile unavyojiona mwenyewe kwa sasa na uhalisia wako/bora wako halisi,ndivyo itakuwa hivyo kwenye maisha yako ya mbele.
👉🏻Pale unapojiona uwezo wako wa sasa wakufanya mambo na tabia inaendana na yule mtu mwenye mafanikio ambaye unaweza kufanana ile uwezo wako wa kujikubali unaongezeka sana.
👉🏻Unapojipenda mwenyewe ni rahisi kujikubali mwenyewe na ndio unapokuwa na furaha na unakuwa na mipango mizuri ya mafanikio.
👉🏻Moja wapo ya tabia nzuri za kuzijenga ni kujiongelesha mwenyewe mambo chanya na mambo ambayo unapenda ya tokee kwako hii inasaidia kujenga utu wako na moja wapo ya neno la muhimu nikusema *najikubali sana*
👉🏻Msingi wa utu *,je dhana yako binafsi inatokea wapi!?*inaanzaje? Na inakuwaje!?
Ukweli ni kwamba kila mtoto anapozaliwa huwa hana hii dhana yake binafsi ingawa dhana hizi hujengwa kulingana na ukoaji kutoka utotoni hadi uzeeni,
Mwanadamu amefundishwa kuamni mambo fulani hii ni kutokana na jamii inayo mzunguka inavyo amini kuhusu mambo fulani
👉🏻Ukweli ni kwamba kila mtoto huwa anazaliwa na karama fulani za kipekee sana, baadhi ya wanasaikolojia wanasema kwamba 60% ya baadhi ya tabia watu huzaliwa nazo mfano ushujaa,kupenda muziki na uwezo wa kukimbia nk,na ndio maana utakuta mtoto mmoja katika familia fulani yeye pekee ndie mwenye uwezo huo ukilinganisha na wengine ingawa wazazi wao ni walewale.
👉🏻Uhalisia bora wa kuzaliwa nao upo katika sehemu mbili;
1.Tulizaliwa bila uoga,ila jamii ndio inatufundisha uoga mfano wazazi ndio wenye kuathiri sana watoto wao kwa kuwapa uogo kuhusu mambo mfano,mzazi atamwogopesha mwanae akimwona nyoka hii inapelekea hata mtoto kuanza kuogopa nyoka ktk maisha yake.
Kuna uogo wa kutoweza kufanya jambo fulani,uoga wa kukataliwa na nk
2.Tulizaliwa tukiwa na uasilia,mwanadamu anapozaliwa huwa tunauasilia wa kulia,kupiga kelele,na kujielezea wenyewe lakini wazazi huwa wanazui watoto kulia wakati fulani,kwa kuwa hakikishia kwamba wasipolia ndio wata wapenda na wakilia hawawapendi watoto,hivyo mtoto hukua kwa kuwa hakikishia wanzake au kutowakiki wenzake mpaka utu uzima hii inabadilisha uasilia wa mtoto na mwanadamu kiujumla!
👉🏻MBINU ZA KUONDOKANA NA UOGA,
Ukweli ni kwamba uoga ulionao na jinsi unavyojikubali huwa vinaenda tofauti,kwa maana nyingine ni kwamba wewe unavyojikubali hivyo ndivyo unapokuwa huogopi kushindwa na kukataliwa!
👉🏻Timiza uwezo wako kamili kwa kusoma sheria hizi nne!
1. *Sheria ya tabia,* ,inasema ikiwa utafanya jambo lolote kwa kurudia rudia basi hufunyika tabia kwako.
2 *.Sheria ya hisia* Inasema kila jambo unalolifanya ni kutokana na hisia ya jambo fulani,hilo jambo huwa ni chanya au ni hasi!
3. *Sheria ya mkusanyiko* inasema Chochote kama utakitilia mkazo na kukikuza na kuongeze kwenye maisha yako basi huwa kinakuwa zaidi.kwa maana nyingine ni kwamba kitu chochote uunapofikiria kwa muda mrefu basi hukua
4. *sheria ya ufanyaji kazi ya akili isiyofikika* inasema akili yako isiyofikika huwa inapokea mawazo, mipango na malengo ambayo yametengenezwa na akili ya kawaida na badae akili isiyo fikika huwa inabadili na kukuhamasisha malengo na mipango kuwa katika uhalisia kwenye maisha yako.
👉🏻Ukweli ni kwamba tabia za mafanikio ni muhimu na pia tabia nzuri ya mafanikio ni pale unapohakikisha akili yako inalenga zaidi kwa yale unayo yahitaji na malengo yako kiujumla
👉🏻Your potential is ulimited and your will be assure of these by taking complete control of your self concept!
DEVELOP YOUR GOOD HABITS,
Ahsante,
usikose kesho sura ya tatu ya kitabu,
Phone.0742364499,
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

Leave a Reply