Kuwa na Mtaji, Kukuza Mtaji

By | June 24, 2018
Kuwa na mtaji ni hatua ya kwanza lakini kukuza mtaji ni swala jingine kabisa .Watu wengi sana wamekuwa na mitaji lakini mitaji yao imekuwa haiongezeki na wakati mwingine mitaji yao imeisha na kusababisha biashara zao kufungwa. Njia zifuatazo zinaweza kukusaidia kukuza mtaji wako wa biashara. 1.Kuongeza mauzo katika biashara (increase sales) Hakuna biashara yoyote inayoweza kukua bila mauzo.Bila kuuza mtaji wako hautaongezeka hata kidogo .Lazima kama tayari umeanzisha biashara yako akili yako uilekeze kuhakikisha kuwa unauza sana kadri iwezekanavyo.Jifunze mbinu mbalimbali za mauzo hata katika nyakati ngumu.Ukiona wewe huuzi bidhaa zako fahamu kuwa watu siyo tatizo wewe ndiwe tatizo .Unaweza kuwa hujui namna ya kuuza bidhaa yako .Jifunze namna ya kuuza . 2.Kuwa na uratibu mzuri wa kumbukumbu za kibiashara (book keeping) Kama umeanza biashara na huna utaratibu wa kutunza kumbukumbu zako za kibiashara kuna hatari kubwa ya kupoteza mtaji wako na mtaji wako hautakua kwa sababau hujui unapata kiasi gani katika biashara yako kwa mwezi ,mwaka ili ikusaidie kuamua ufanye nini katika biashara yako. Ni vema ukawa na utaratibu wa kutunza kumbukumbu za kibiashara vizuri ili zikusaidie kuratibu fedha zinazopatikana kwenye biashara yako . 3.Usitoe fedha ya biashara yako kwenye mzunguko Ili mtaji wako ukue ni muhimu sana fedha za biashara yako zisitoke kwenye mzunguko .Usile mtaji wako kwa kufanya hivyo unaua biashara yako .Acha fedha inayopatikana kwenye biashara yako iendelee kuzunguka kadri iwezekanavyo . Watu wengi wamekuwa wakitumia fedha zao za biashara kununua mahitaji yao binafsi na kwa kufanya hivyo wamejikuta wakiua biashara zao . 4.Tafuta mtu wa kuungana mfanye biashara (Parternship) Hii ni njia nyingine ya kukuza mtaji .Kama unaona mtaji wako ni mdogo na wazo lako linahitaji mtaji mkubwa ,unaweza kumtafuta mtu unayemwamini mkaungana kufanya biashara fulani kwa makubaliano ya kisheria . Mkiungana wawili au hata zaidi nguvu inaongezeka.Kwa bahati mbaya kuwapata watu waaminifu wa kufanya nao biashara imekuwa ngumu sana 5.Uza wazo lako (Sale your idea) Kuna mtu anakuwa na wazo lakini hana mtaji au mtaji wake ni mdogo .Mtu huyu anaweza kuuza wazo lake na kuna watu wako tayari kuwekeza kwenye mawazo ya watu kwa makubaliano ya kisheria. 6.Uza hisa zako (sale your shares) Unaweza kuwa umeshaanzisha kampuni au biashara na mtaji wako ukawa siyo mkubwa sana .Kuuza hisa za kampuni yako ni njia nyingine ambayo unaweza kuitumia . Hisa maana yake unaruhusu watu kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni au biashara yako kwa makubaliano fulani ambao watakuwa wanapata gawio la faida ya kampuni au biashara yako kila mwaka .Kama kampuni inapata hasara .Wote mnapata hasara. Kopa Fedha* Hii ni njia nyingine ya kukuza mtaji japo watu wengi waliokopa waliposhindwa kurejesha mkopo wao taasisi nyingi za fedha zilifilisi biashara zao. Siku hizi siyo lazima ukope benki maana benki nyingi zina riba kubwa .Unashauriwa kujiunga na vikundi ambavyo vinakopesha fedha .Jiunge na SACCOS ambayo unaona unaweza kujiunga.Jiunge na VICOBA au vikundi vya ukopeshaji .Kwanini ujiunge?? Unashauriwa kujiunga ili uweze kuwa na sifa ya kukopa fedha ambazo unaweza kutumia kukuza mtaji wako wa biashara .
Tatizo kubwa kwa sisi wanavyuo hatuwazi nje ya box,kila mtu akipata vilaki kadhaa(mwanachuo) anakimbilia kufungua banda la chipsi.OK fine malengo yako baada ya hilo banda?.
Ok Mimi ni mwanachuo wa mwaka wa pili,nimeamua kuja na ubunifu tofauti wa biashara yangu.Nimendunduliza nikafikisha laki sita na nusu na ninadream zakuja kuwa bakharesa hapo baadae.Unajua nimefanya nini?.
Nimetafuta vijana waaminifu wawili niliosoma nao wakafeli school.Mmoja yupo huko hom(mkoani) mwingine nimemtumia nauli elfu 50 aje dsm nikae nae geto(kashafika).
Nimechofanya yule wa mkoani(ninamuamini sana) nilimtumia laki nne na nusu,akanunua mchele kg 400.kilo kwa sasa mchele mpya ni 1000Tzsh.Kwahiyo apo ilienda sh laki nne.akabakiwa na sh elfu arobain,nmejumlisha na hela yakutoa mchele mashineni na magunia yakuuwekea.
Baada ya hapo akaenda tafuta usafiri ambao kila kg 100,wamemtoza sh elfu 10000.kwahiyo kg 400 akawa kamaliza ela mpaka mzigo kufika dar.
Sasa unajua nmeamua kuifanya vipi hii biashara.Mimi nauza kuanzia Kg 5. Kwa shilling 1800 kila kilo.Nmechukua oda ya mama ntilie wanao uza chakula chuo nacho somea,pia na baadhi ya mama ntilie wamtaani.
Pia nawauzia wanafunzi wanaojipikia kwenye magheto.Jambo la msingi nimelofanya nikuwa mtu akihitaji mchele ananipigia simu nampelekea mchele mpaka mahali anapokaa.
Kama itakuwa mbali sana ambapo nitahitaji usafiri basi itabidi kg1 mteja ainunue kwa sh 1900.
Mchele ninaouza quality yake kwenye maduka ya mitaani ni sh 2200.
Sasa nimeanza na hizi kg 400,ambazo nikiziuza kwa kg1, sh 1800. Nitatoa sh 720000.Na hii nategemea ndani ya siku 10, mpaka 12 nitakuwa nimeshaipata, kwahiyo awamu ijayo nitatuma kg zaidi ya 580 kama bei haitopanda
Tumekubaliana nahawa jamaa zangu wawili tutaanza kulipana japo hela ya sabuni baada ya miezi minne.Na huku nikiwa nimesubiri hela ya bum nitoe kama laki tatu niongezee ili mtaji ukue baada ya mauzo.
Pia nimekopa mizani nitakuwa nalipa kidogo kidogo kadiri mauzo yangu yatakavyokuwa.
Chakula ambacho nakula mie na huyu jamaa yangu kipo nje ya bajeti ya mtaji.
Na wewe mwanafunzi mahali ulipo/mtu mwenye mtaji mdogo waweza jaribu hii nahakika itakulipa.

Au kama mtu yeyote mwenye ushauri zaidi namna nitakavyoboresha zaidi anaweza kunisaidia(tusaidia

Leave a Reply